Revelation 1:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Nguvu, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mwenyezi Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana Mungu asema, “Mimi ni Alfa na Omega. Mimi ndiye niliyepo, aliyekuwepo na anayekuja. Mimi ni Mwenye Uwezo Wote.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Nguvu, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mwenyezi Mungu, “aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Nguvu, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi ni A na O, ni kwamba: Mwanzo na Mwisho; ndivyo, Bwana Mungu anavyosema aliopo, aliyekuwapo, atakayekuja, aliye Mwenyezi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana Mungu Mwenye Uwezo anasema: “Mimi ni Alfa na Omega.” Ni yeye anayekuwa, aliyekuwa na anayekuja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.