Revelation 1:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi ni Yohane, ndugu yenu, ambaye kwa kuungana na Yesu, nashiriki pamoja nanyi mateso na ufalme wake na uvumilivu thabiti. Mimi nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo kwa sababu ya kuhubiri neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi, Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Isa na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mimi ni Yohana, mwamini mwenzenu. Tuko pamoja katika Yesu na tunashirikiana mambo haya: mateso, ufalme na uvumilivu wenye subira. Nilikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa sababu nimekuwa mwaminifu kwa ujumbe wa Mungu na kwa ajili ya kweli ya Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi ni Yohane, ndugu yenu; na kwa kuungana na Kristo nashiriki pamoja nanyi katika kustahimili mateso yanayowapata wale walio wa Utawala wake. Mimi nilikuwa kisiwani Patmo kwa sababu ya kuhubiri ujumbe wa Mungu na ukweli wa Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi ni Yohane, ndugu yenu, ambaye kwa kuungana na Yesu, nashiriki pamoja nanyi mateso na ufalme wake na uvumilivu thabiti. Mimi nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo kwa sababu ya kuhubiri neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi, Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Yesu na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi, Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Isa na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi ni Yohane, ndugu yenu, ambaye kwa kuungana na Yesu, nashiriki pamoja nanyi mateso na ufalme wake na uvumilivu thabiti. Mimi nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo kwa sababu ya kuhubiri neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenzenu wa maumivu na wa ufalme na wa uvumilivu, tupewao na Yesu, nilikuwa katika kisiwa kinachoitwa Patimo. Nilikuwako, maana nalilitangaza Neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ni ndugu yenu Yoane. Kwa njia ya kuungana na Yesu, ninashirikiana nanyi katika mateso, katika ufalme wake na katika kuvumilia. Mimi nilikuwa nimepelekwa katika kisanga kinachoitwa Patimo, kwa sababu nilihubiri Neno la Mungu na ukweli ulioshuhudiwa na Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.