Revelation 10:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akaapa kwa Yule aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo, akasema, “Hakuna kungoja tena!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika akaapa kwa nguvu ya yule aishiye milele na milele. Ndiye aliyeziumba mbingu na vyote vilivyomo ndani yake. Aliumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, na aliumba bahari na vyote vilivyomo ndani yake. Malaika alisema, “Hakutakuwa kusubiri tena!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akaapa kwa Jina la Mungu aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo ndani yake, akasema, “Hakuna kungoja tena!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akaapa kwa Yule aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo ndani yake, akasema, “Hakuna kungoja tena!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na kukawia tena baada ya haya;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akaapa na kumtaja yeye aliye Mwenye uzima kale na kale pasipo mwisho, aliyeziumba mbingu navyo vilivyomo ndani yake, hata nchi navyo vilivyomo ndani yake, hata bahari navyo vilivyomo ndani yake, akisema: Hapatakuwa siku tena,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaapa kwa jina la Mungu anayeishi kwa milele na milele, muumba wa mbingu na vitu vyote vinavyokuwa ndani yake, nayo dunia na vyote vinavyokuwa ndani yake, pamoja na bahari na vitu vyote vinavyokuwa ndani yake, na kusema: “Hakutakuwa tena muda unaobaki!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya,