Revelation 10:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wakati yule malaika wa saba atakapotoa sauti ya tarumbeta yake, Mungu atakamilisha mpango wake wa siri kama alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini katika siku zile huyo malaika wa saba atakaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa, kama vile alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika siku ambazo malaika wa saba atakuwa tayari kupuliza tarumbeta yake, mpango wa siri wa Mungu utakamilika, nao ni Habari Njema ambayo Mungu aliwaambia watumishi wake, manabii.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wakati ule malaika wa saba atakapotoa sauti yake, wakati atakapopiga tarumbeta yake, Mungu atakamilisha mpango wake wa siri kama alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wakati yule malaika wa saba atakapotoa sauti ya tarumbeta yake, Mungu atakamilisha mpango wake wa siri kama alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini katika siku zile ambazo huyo malaika wa saba atakapokaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa, kama vile alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini katika siku zile ambazo huyo malaika wa saba atakapokaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa, kama vile alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowatangazia watumishi wake hao manabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wakati yule malaika wa saba atakapotoa sauti ya tarumbeta yake, Mungu atakamilisha mpango wake wa siri kama alivyowatangazia watumishi wake manabii.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila siku ya sauti ya malaika wa saba, atakapopiga baragumu, ndipo, patakapotimia fumbo la Mungu, kama alivyowapigia mbiu njema wale wafumbuaji waliokuwa watumwa wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakati malaika wa saba atakapopiga baragumu, Mungu atatimiza mipango yake aliyoficha sawa vile alivyotangaza kwa kinywa cha manabii waliomutumikia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
isipokuwa katika siku zile za malaika wa saba, atakapokuwa tayari kupiga: hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowakhubiri watumishi wake manabii.