Revelation 10:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni pale awali ikasema nami tena: “Nenda ukakichukue kile kitabu kilichofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaika asimamaye juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena, ikaniambia, “Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikasikia tena sauti ile ile kutoka mbinguni. Ikaniambia, “Nenda ukachukue kitabu kilicho wazi mkononi mwa malaika, aliyesimama juu ya bahari na nchi kavu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni pale awali ikasema nami tena: “Nenda ukakichukue kile kitabu kilichofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaika asimamaye juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni pale awali ikasema nami tena: “Nenda ukakichukue kile kitabu kilichofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaika asimamaye juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena ikaniambia, “Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena ikaniambia, “Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Nenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni pale awali ikasema nami tena: “Nenda ukakichukue kile kitabu kilichofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaika asimamaye juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, ile sauti, niliyoisikia toka mbinguni, iliposema tena nami kwamba: Nenda, ukitwae kile kitabu kidogo kilichokuwa kimefunuka, kilichomo mkononi mwa malaika aliyesimama mguu mmoja baharini na mmoja nchini!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikasikia tena sauti kutoka mbinguni ikiniambia: “Kwenda utwae kile kitabu kidogo chenye kufunguliwa katika mukono wa yule malaika anayesimama juu ya bahari na juu ya inchi kavu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, kitwae kile kitabu kidogo kilichofunuliwa katika mkono wa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya inchi.