Revelation 11:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, “Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani na kawahesabu watu wanaoabudu ndani ya hekalu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo nikapewa mwanzi uliokuwa kama ufito wa kupimia, nikaambiwa, “Nenda ukapime Hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nilipewa fimbo ya kupimia, ndefu kama fimbo ya kutembelea. Nikaambiwa, “Nenda ukalipime hekalu la Mungu na madhabahu na uwahesabu watu wanaoabudu humo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, “Inuka, ukalipime Hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani, na ukawahesabu watu wanaoabudu ndani ya Hekalu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, “Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani na kawahesabu watu wanaoabudu ndani ya hekalu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo nikapewa mwanzi wa kupimia ulio kama fimbo, nikaambiwa, “Nenda ukapime Hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo nikapewa mwanzi uliokuwa kama ufito wa kupimia, nikaambiwa, “Nenda ukapime hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wanaosujudu humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha kupimia, nikaambiwa, “Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, madhabahu ya kufukizia ubani na kawahesabu watu wanaoabudu ndani ya hekalu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikapewa mwanzi uliofanana na fimbo, nikaambiwa: Inuka, ulipime Jumba la Mungu na meza ya Bwana nao wenye kutambikia mlemle!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wakanipa fimbo ya kupima urefu na kuniambia: “Simama upime hekalu la Mungu pamoja na mazabahu na kuwahesabu watu wanaoabudu ndani yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NIKAPEWA mwanzi kama ufito mmoja, akaniambia, Inuka, ukaipime hekalu ya Mungu, na madhbabu, nao wasujuduo humo.