Revelation 11:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi, maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wanaoishi duniani watazitazama maiti za hao manabii wawili kwa furaha, na kushangilia kwa kupeana zawadi, kwa sababu hao manabii waliwatesa watu wanaoishi duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Kila aishiye duniani atafurahi kwa sababu mashahidi hawa wawili wamekufa. Watu watafanya sherehe na kupeana zawadi kwa sababu manabii hawa wawili walileta mateso mengi kwa watu waishio duniani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi, maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu waishio duniani watafurahia kifo cha hao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadi, maana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua mno watu wa dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wakaao nchini watashangilia kwa ajili yao na kupiga vigelegele na kupelekeana matunzo, kwa sababu wafumbuaji wale wawili waliwatesa wakaao nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wa dunia watafurahi kwa ajili ya kifo chao na kushangilia. Watatumiana zawadi, kwa maana manabii hawa wawili waliwasumbua sana wakaaji wa dunia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wakaao juu ya inchi watafanya furaha juu yao ua kushangilia. Na watapelekeana zawadi kwa kuwa manabii hawo wawili waliwatesa wao wakaao juu ya inchi.