Revelation 11:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui zao wakiwa wanawatazama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njooni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha mashahidi wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikisema, “Njooni huku juu!” Na wote wawili wakaenda juu mbinguni katika wingu, adui zao wakiangalia wanavyokwenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui wao wakiwa wanawatazama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui zao wakiwa wanawatazama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njooni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, hao manabii wawili wakasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Nao wakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui zao wakiwa wanawatazama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakasikia sauti kuu toka mbinguni iliyowaambia: Pandeni huku! Walipopanda mbinguni katika wingu, wachukivu wao walikuwa wanawatazama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manabii hao wawili wakasikia sauti kubwa toka mbinguni ikiwaambia: “Mupande huku!” Wakapanda mbinguni wakizungukwa na wingu, wale waadui zao wakiwa wakiwaangalia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hatta huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.