Revelation 11:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Saa hiyo hiyo, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika wakati huo huo kulitokea tetemeko kuu la ardhi. Sehemu ya kumi ya mji ikateketea, na watu elfu saba wakafa. Wale ambao hawakufa waliogopa sana. Wakampa utukufu Mungu wa mbinguni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu elfu saba wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliobakia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Saa ileile pakawa tetemeko kubwa la nchi, nalo fungu la kumi la mji likafudikizwa, watu waliouawa na hilo tetemeko la nchi majina yao yalikuwa 7000. Nao waliosalia wakashikwa na woga, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na saa ile ile, kukatokea tetemeko kubwa la inchi, na sehemu moja ya kumi ya muji ikabomoka, na watu elfu saba wakakufa katika tetemeko lile. Watu waliobaki wakashikwa na hofu, nao wakamutukuza Mungu wa mbinguni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.