Revelation 11:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa ufalme wa ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Al-Masihi wake, naye atatawala milele na milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa saba alipopuliza tarumbeta yake, zikatokea sauti kuu mbinguni, zikasema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Masihi wake sasa. Na atatawala milele na milele.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa utawala juu ya ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa ufalme wa ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Mungu wetu Mwenyezi na wa Al-Masihi wake, naye atatawala milele na milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa ufalme wa ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Malaika wa saba alipopiga baragumu, kukawa na sauti kuu nyingi mbinguni zikisema: Ufalme wa ulimwengu umekwisha kuwa wake Bwana wetu na wa Kristo wake; ndiye atakayetawala kale na kale pasipo mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha malaika wa saba akapiga baragumu. Halafu sauti kubwa zikasikilika katika mbingu, zikisema: “Sasa utawala juu ya dunia ni wa Bwana wetu na wa Masiya wake. Naye atatawala kwa milele na milele!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.