Revelation 11:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya utawala, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha wazee 24 wakaanguka chini nyuso zao zikiwa chini wakamwabudu Mungu. Hawa ni wazee ambao wanakaa kwenye viti vyao vya heshima mbele za Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mwenyezi Mungu, kwenye viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi, wakamsujudia Mungu
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wale wazee 24 waliokaa mbele ya Mungu katika viti vyao vya kifalme walipoanguka nyusoni pao, wakamsujudia Mungu
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wale wazee makumi mbili na wane wanaokaa juu ya viti vyao vya kifalme mbele ya Mungu, wakainama uso mpaka chini wakimwabudu Mungu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale wazee ishirini na wane waketio mbele ya Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifudifudi, wakamsujudu Mungu,