Revelation 11:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mataifa walikasirika; nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa, na kuwapa thawabu watumishi wako manabii, na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mataifa walikasirika, lakini sasa ni wakati kwa ajili ya hasira yako. Sasa ni wakati wa waliokufa kuhukumiwa. Ni wakati wa kuwapa thawabu watumishi wako, manabii, na kuwapa thawabu watu wako watakatifu, wakubwa na wadogo, wanaokuheshimu wewe. Ni wakati wa kuwaangamiza watu wanaoiangamiza dunia!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wa mataifa waliwaka hasira, maana wakati wa ghadhabu yako umefika, wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watu wako na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mataifa walikasirika kwa kuwa wakati wa ghadhabu Yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina Lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mataifa walikasirika nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumishi wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamizimu walipopatwa na makali ndipo, makali, yako yalipotokea, ndipo, siku yako ilipotimia ya kuwahukumu wafu na ya kuwapokeza watumwa wako walio wafumbuaji nao watakatifu nao walioliogopa Jina lako, walio wadogo nao walio wakubwa. Siku imetimia ya kuwaangamiza wenye kuiangamiza nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa mataifa mengine walikasirika, lakini kasirani yako imetokea. Sasa ni wakati wa kuhukumu waliokufa, nao wakati wa kuwapa waliokutumikia zawadi, ndio manabii wako, na wote wanaoheshimu jina lako, wakubwa na wadogo. Ni wakati wa kuangamiza wale wanaoharibu dunia!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.