Revelation 11:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana hekaluni mwake. Kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana humo. Kukatokea miali ya radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la ardhi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa. Sanduku la Agano likaonekana ndani ya hekalu lake. Kisha kukatokea miali ya radi na miungurumo ya radi, kelele, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana Hekaluni mwake. Kisha kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana hekaluni mwake. Kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa na Sanduku la Agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana hekaluni mwake. Kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Jumba la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, mkaonekana mlemle Jumbani mwa Mungu Sanduku la Agano lake. Kukapiga umeme na uvumi na ngurumo, kukawa na tetemeko la nchi na mvua nyingi sana ya mawe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha hekalu la Mungu linalokuwa mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Agano lake likaonekana ndani yake. Halafu kukatokea umeme, makelele, ngurumo ya radi, tetemeko la inchi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.