Revelation 11:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa. Jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Isa Bwana wao alisulubiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Miili ya mashahidi hawa wawili italala kwenye mtaa wa mji mkuu. Mji huu unaitwa Sodoma na Misri. Majina ya mji huu yana maana maalumu. Huu ni mji ambako Bwana aliuawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa; jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa. Jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Bwana wao alisulibiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Isa Bwana wao alisulubiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maiti zao zitabaki katika barabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa. Jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mizoga yao itakaa katika njia ya mji ule mkubwa unaoitwa kiroho Sodomu na Misri; ndipo, naye Bwana wao alipowambwa msalabani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maiti zao zitabaki katika barabara ya muji ule mukubwa unaoitwa kwa fumbo Sodoma au Misri. Ni ndani ya muji ule Bwana wao alitundikwa juu ya musalaba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.