Revelation 12:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji lenye nyota kumi na mbili lilikuwa kichwani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jambo la ajabu lilionekana mbinguni: Mwanamke aliyevalishwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake alionekana. Alikuwa na taji yenye nyota kumi na mbili kichwani pake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha ishara kubwa ikaonekana mbinguni. Palikuwa hapo mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ukiwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha kukaonekana kielekezo kikubwa mbinguni: mwanamke aliyekuwa amevikwa jua alikuwa anao mwezi chini miguuni pake, napo kichwani pake alikuwa na kilemba cha nyota kumi na mbili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kukaonekana kitambulisho kikubwa mbinguni. Kulikuwa mwanamuke aliyekuwa amefunikwa na jua, na mwezi chini kwenye miguu yake. Na juu ya kichwa kulikuwa taji lenye nyota kumi na mbili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara.