Revelation 12:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: “Sasa umefika ukombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: “Sasa wokovu na uweza na ufalme wa Mungu wetu Mwenyezi umekuja, na mamlaka ya Al-Masihi wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nilisikia sauti kubwa mbinguni ikisema: “Ushindi na uweza na ufalme wa Mungu wetu na mamlaka ya Masihi wake umekuja sasa, kwa sababu mshitaki wa kaka na dada zetu ametupwa chini. Ndiye aliyewashitaki kwa Mungu, mchana na usiku.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: “Sasa ukombozi utokao kwa Mungu umefika! Nguvu na Utawala wa Mungu wetu umedhihirika. Na Kristo wake ameonyesha mamlaka yake! Maana yule mdhalimu wa ndugu zetu, aliyesimama mbele ya Mungu akiwashtaki usiku na mchana, sasa ametupwa nje.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: “Sasa umefika ukombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: “Sasa Wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: “Sasa wokovu na uweza na Ufalme wa Mwenyezi Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Al-Masihi wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: “Sasa umefika ukombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: Sasa wokovu na uwezo na ufalme umekuwa wa Mungu wetu, nazo nguvu zimekuwa zake Kristo wake, kwani msutaji wa ndugu zetu amebwagwa nchini; ndiye aliyewasuta mbele ya Mungu wetu mchana na usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni, ikisema: “Sasa wokovu, uwezo na ufalme wa Mungu, na mamlaka ya Kristo wake vimefika. Ni vile, kwa yule aliyekuwa akiwashitaki wandugu zetu mbele ya Mungu wetu muchana na usiku ametupwa chini ya mbingu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikinena, Sasa kumekuwa wokofu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake: kwa maana ametupwa mshitaki wa ndugu zetu, awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchaua na nsiku.