Revelation 12:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto wa kiume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Joka alipoona amekwisha tupwa chini duniani, alimkimbiza mwanamke aliyemzaa mtoto wa kiume.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanamume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanaume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na joka lile lilipoona ya kuwa limetupwa katika nchi, lilimfuatia mwanamke yule aliyemzaa mtoto wa kiume.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule joka alipoona, ya kuwa amebwagwa nchini, ndipo, alipomkimbiza yule mwanamke aliyemzaa yule mtoto wa kiume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati yule nyoka alipotambua kwamba ametupwa katika dunia, akaanza kumufuatilia yule mwanamuke aliyezaa mutoto mwanaume.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika inchi alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.