Revelation 12:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka hadi mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko jangwani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu, ya wakati ambako lile joka haliwezi kufika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mwanamke alipewa mabawa mawili ya tai mkuu. Aliweza kuruka mpaka mahali palipoandaliwa kwa ajili yake jangwani. Huko atatunzwa kwa muda wa miaka mitatu na nusu akiwa mbali na joka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali, pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko nyikani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu, wakati ambako yule joka hawezi kufika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko jangwani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu, ya wakati ambako yule joka hawezi kufika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwanamke akapewa mabawa mawili ya yule tai mkibwa, aende nyikani na kuruka, apafikie mahali pake, anapolishwa siku hizi nazo zitakazokuja nacho kipande cha siku zitakazosalia, atoke usoni pake yule joka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yule mwanamuke akapewa mabawa mawili yanayokuwa kama ya tai, kusudi apate kuruka kwenda katika jangwa kwenye nafasi aliyotengenezewa, mbali na yule nyoka. Na kule apate kukulishwa kwa muda wa miaka mitatu na nusu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwanamke yule akapewa mabawa mawili kama ya tai yule mkubwa, illi aruke, aende zake nyikani hatta mahali pake, bapo alishwapo wakati na nyakati na nussu ya wakati, mbali ya nyoka huyo.