Revelation 12:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: Ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao lile joka lilikuwa limeutoa kinywani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini nchi ilimsaidia mwanamke. Nchi ilifungua kichwa chake na kumeza mto uliotoka kwenye kinywa cha joka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule lililoutoa lile joka katika kinywa chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: Ikajifunua kama mdomo na kuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nchi ikamsaidia yule mwanamke, maana hiyo nchi ikakifumbua kinywa chake, ikaunywa ule mto, yule joka alioutoa kinywani mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini udongo ukamusaidia yule mwanamuke; ukabomoka kama vile kinywa na kumeza ule muto uliotoka katika kinywa cha yule nyoka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Inchi ikamsaidia mwanamke, inchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.