Revelation 12:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na wazawa waliosalia wa huyo mwanamke, yaani wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Isa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha joka lilimkasirikia sana mwanamke. Likaenda kufanya vita na watoto wake wengine. Watoto wa mwanamke ni wale wanaozitii amri za Mungu na wanayo kweli ambayo Yesu aliifundisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kuuzingatia ukweli wa Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Isa Al-Masihi. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazao wake waliobakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; nalo likasimama juu ya mchanga wa bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, joka hilo likamkasirikia huyo mama, likajiondokea, likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama, yaani wote wanaotii amri za Mungu na kumshuhudia Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo yule joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake kufanya vita nao waliosalia wa uzao wake, ndio wale walioyashika maagizo yake Mungu, waliofuliza kumshuhudia Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule nyoka akamukasirikia yule mwanamuke na kwenda kufanya vita na wazao wake wengine; ndio wale wanaoshika amri za Mungu na kufuata ukweli ulioshuhudiwa na Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Joka akamkasirikia mwanamke akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo.