Revelation 12:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini joka hilo na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini joka na malaika wake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi yao huko mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
lakini joka na malaika zake hawakuwa na nguvu za kutosha kushinda, na hivyo wakapoteza nafasi zao mbinguni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini joka hilo halikuweza kuwashinda, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini joka hilo na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini joka na malaika zake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini joka na malaika zake wakashindwa, na hapakuwa tena na nafasi yao huko mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini joka hilo na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hawakushinda, tena hapakuonekana mahali pao pa kukaa mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini akashindwa na haikuwezekana tena kwake kukaa mbinguni pamoja na wamalaika zake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nao bawakushinda wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.