Revelation 13:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari. Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake, na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha niliona mnyama mwenye pembe kumi na vichwa saba akipanda kutoka baharini. Kila pembe yake ilikuwa na taji. Alikuwa na kumkufuru Mungu lililoandikwa kwenye kila kichwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
(G12-18) Na likajisimamia ukingoni mwa bahari. (G13-1) Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari. Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari. Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake, na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, alikuwa na pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya kukufuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juu ya vichwa hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaona nyama mkali, akitoka baharini mwenye pembe kumi na vichwa saba; juu hizo pembe zake zilikuwa na vilemba kumi vya kifalme, napo vichwani pake palikuwa na majina ya kumtukana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona nyama mumoja wa ajabu akitokea ndani ya bahari. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Na juu ya kila pembe lake kulikuwa taji, na juu ya vichwa vile kulikuwa kumeandikwa jina la kumutukana Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NIKASIMAMA juu ya mchanga wa bahari. Nikaona nyama akitoka katika bahari niwenye vichwa saba, na pembe kumi, na juu ya pembe zile vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya ukafiri.