Revelation 13:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga.” Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeyote ambaye ni lazima awe mfungwa, atakuwa mfungwa. Yeyote ambaye ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hii inamaanisha kwamba watakatifu wa Mungu lazima wawe na subira na imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Waliokusudiwa kuchukuliwa mateka lazima watatekwa; waliokusudiwa kuuawa kwa upanga lazima watauawa kwa upanga. Kutokana na hayo ni lazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu na imani.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye wito kwa ajili ya saburi na imani ya watakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka, atachukuliwa mateka. Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye wito wa subira na imani ya watakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliyepangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa; wa kuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo, watu wa Mungu na wawe na uvumilivu na imani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama yuko mwenye kuteka, naye atatekwa; kama yuko mwenye kuua kwa upanga, naye sharti auawe kwa upanga. Hapo ndipo, watakatifu watakapovumilia kwa kumtegemea Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yule aliyekusudiwa kuwa mufungwa, atafungwa; na yule aliyekusudiwa kuuawa kwa upanga, atauawa kwa upanga. Kwa sababu hiyo, watu wa Mungu wanapaswa kuwa wavumilivu na wenye imani.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu.