Revelation 13:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapa panatakiwa hekima! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni 666.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni mia sita sitini na sita (666).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mwenye uelewa anaweza kujua maana ya namba ya mnyama. Hili linahitaji hekima. Namba hii ni namba ya mtu. Nayo ni 666.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapa ni lazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni mia sita sitini na sita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapa panatakiwa hekima! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni 666.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapa panatakiwa hekima! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni 666.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapa ndipo panapotakwa werevu wa kweli; aliye mwenye akili na akifumbue kiwango cha yule nyama! Nacho kiwango chake ndicho mia sita na sitini na sita (666).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapa inafaa kuwa na hekima. Yule anayekuwa na akili afafanue hesabu ya tarakimu zinazolingana na jina la yule nyama, kwa maana tarakimu ile ni ya mutu fulani. Nayo ni mia sita makumi sita na sita.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapo udipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya nyama huyo: maana ni hesabu ya mwana Adamu; na hesabu yake ni Sita mia, sittini na sita.