Revelation 13:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kichwa kimoja cha mnyama kilionekana kama kimejeruhiwa na kuuawa, lakini kidonda cha mauti kilipona. Watu wote ulimwenguni walishangaa, na wote walimfuata mnyama.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kimojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kimojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaona kimojawapo cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miongoni mwa vichwa vyake nikaona kimoja kilichokuwa, kama kimepasuliwa kwa kuuawa, lakini donda lake la kuuawa lilikuwa limepona. Ulimwengu wote ukamtazama yule nyama na kumstuka,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kimoja cha vichwa vya yule nyama kilionekana kwamba kilikuwa kimeumizwa vibaya sana, lakini kidonda kilichokuwa cha hatari ya kufa kilikuwa kimekwisha kupona. Na kwa hiyo watu wote wa dunia wakashangaa na kumufuata yule nyama.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimejeruhi jeraha ya mauti. Pigo lake la mauti likaponywa, dunia yote ikastaajabu nyama ya nyama yule.