Revelation 13:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu waliliabudu joka kwa sababu limempa nguvu mnyama, na pia walimwabudu mnyama. Waliuliza, “Nani ana nguvu kama mnyama? Nani anaweza kufanya vita dhidi yake?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakalisujudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha wakamwangukia yule joka, kwa sababu alimpa yule nyama nguvu zake, wakamwangukia naye yule nyama wakisema: Yuko nani anayefanana na nyama huyu? Tena yuko nani anayeweza kupiga vita naye?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakaanza kumwabudu yule nyoka kwa sababu alimupa yule nyama uwezo wake. Vilevile wakamwabudu yule nyama, wakisema: “Ni nani anayefanana na nyama huyu? Ni nani anayeweza kupigana vita naye?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamsujudu yule joka aliyempa nyama uwezo, wakamsujudu yule nyama, wakisema, Nani afananae na nyama? Nani awezae kufanya vita nae?