Revelation 13:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arubaini na miwili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo mnyama akapewa mdomo wa kusema maneno ya kiburi na kukufuru, na uwezo wa kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnyama aliruhusiwa kujigamba na kumtukana Mungu na kutumia nguvu zake kwa miezi arobaini na mbili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arubaini na miwili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo mnyama akapewa kusema maneno ya kujisifu na kukufuru na kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo mnyama akapewa kusema maneno ya kiburi na kukufuru na kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya kukufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arubaini na miwili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akapewa domo la kusema makuu ya kumtukana Mungu, akapewa nguvu ya kuyafanya hayo mambo yake miezi 42.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule nyama akapewa uwezo wa kusema maneno ya kiburi ya kumutukana Mungu. Naye akapewa mamlaka ya kufanya kazi yake kwa muda wa miezi makumi ine na miwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akapewa kinywa kunena maneno makuu, ya ukafiri. Akapewa uwezo kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili.