Revelation 13:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao watu wote wanaoishi duniani watamwabudu huyo mnyama: wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila anayeishi duniani angemwabudu mnyama. Hawa ni watu wote ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo tangu mwanzo wa ulimwengu. Mwanakondoo ndiye yule aliyeuawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo aliyechinjwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo watamwangukia yeye wote wakaao nchini, ambao tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa, hawakuandikwa majina yao katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wote wa dunia watamwabudu, ndio wale wote ambao tangia kuumbwa kwa dunia, majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.