Revelation 14:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikaona mlima Siyoni na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu 144,000 ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikatazama, na hapo mbele yangu Mwana-Kondoo alikuwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale elfu mia moja na arobaini na nne wenye jina la Mwana-Kondoo na jina la Baba yake limeandikwa kwenye paji za nyuso zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikatazama, na mbele yangu alikuwepo Mwanakondoo, amesimama juu ya Mlima Sayuni. Watu 144,000 walikuwa pamoja naye. Jina lake na la Baba yake yalikuwa yameandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikaona mlima Sioni, na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu mia moja arobaini na nne elfu ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikaona mlima Siyoni na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu 144,000 ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arobaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikaona mlima Siyoni na Mwanakondoo amesimama juu yake; pamoja naye walikuwa watu 144,000 ambao juu ya paji za nyuso zao walikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina la Baba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikamwona Mwana kondoo, akisimama mlimani kwa Sioni juu. Pamoja naye kulikuwako watu 144000 waliokuwa wameandikwa Jina lake na Jina la Baba yake mapajini pao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaangalia, nikaona Mwana-Kondoo akisimama juu ya mulima Sayuni. Naye alikuwa pamoja na watu elfu mia moja makumi ine na ine, na juu ya paji za nyuso za watu wale kulikuwa kumeandikwa jina lake na jina la Baba yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.