Revelation 14:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, ni lazima watu wa Mungu, yaani wale wanaotii amri za Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapa ndipo penye wito wa subira na uvumilivu wa watakatifu; wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu katika uaminifu kwa Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii inamaanisha kuwa ni lazima watakatifu wa Mungu wawe na subira. Ni lazima wazitii amri za Mungu nakuendelea kumwamini Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kutokana na hayo, ni lazima watu wa Mungu, yaani watu wanaotii amri ya Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, ni lazima watu wa Mungu, yaani wale wanaotii amri za Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapa ndipo penye subira na uvumilivu wa watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hapa ndipo penye wito wa subira na uvumilivu wa watakatifu; wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu katika uaminifu kwa Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, ni lazima watu wa Mungu, yaani wale wanaotii amri za Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapa ndipo, watakatifu watakapovumilia, wayashikao maagizo ya Mungu wakifuliza kumtegemea Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo, watu wa Mungu wanaoshika amri za Mungu na kumwamini Yesu wanapaswa kuwa wavumilivu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.