Revelation 14:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema, “Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wafu wafao katika Isa Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho wa Mungu, “watapumzika kutoka taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni, ikasema, “Liandike hili: Kuanzia sasa heri wale wanaokufa wakiwa wa Bwana.” Roho Mtakatifu anasema, “Ndiyo, hilo ni kweli. Watapumzika kutokana na kazi yao ngumu. Yale waliyotenda yatakaa pamoja nao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema, “Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema, “Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wafu wafao katika Isa Bwana tangu sasa.” “Naam,” asema Roho, “watapumzika kutoka taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema, “Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matunda ya jasho lao yatawafuata.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikasikia sauti toka mbinguni, ikisema: Andika: Wenye shangwe ni wafu waliokufa na kumtegemea Bwana tangu sasa. Kweli Roho anasema: Huyapumzikia masumbuko yao, kwani matendo yao hufuatana nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena nikasikia sauti kutoka mbinguni, ikisema: “Andika maneno haya: ‘Heri tangu sasa kwa watu wanaokufa wakimwamini Bwana!’ ” Naye Roho anasema: “Ndiyo, ni kweli. Watapumzika toka katika masumbuko yao, kwa maana matendo yao yatafuatana nao.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.