Revelation 14:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha malaika mwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuni, akamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenye mundu wenye makali, “Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na malaika mwingine, aliyekuwa msimamizi wa moto wa madhabahu akatoka madhabahuni. Akamwita malaika mwenye mundu mkali na kusema, “Chukua mundu wako wenye makali na ukusanye mafungu ya zabibu kutoka shamba la mizabibu duniani. Zabibu zimeiva duniani.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika mwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuni akamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenye mundu wenye makali, “Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha malaika mwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuni, akamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenye mundu wenye makali, “Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha malaika mwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuni, akamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenye mundu wenye makali, “Nawe tia huo mundu wako mkali, ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakatoka na malaika mwingine penye meza ya Bwana; yeye alikuwa na nguvu ya moto, akapiga sauti kuu ya kumwambia mwenye mndu mkali akisema: Tuma mndu wako mkali, uvichume vichala vya mizabibu ya nchini, kwani zabibu zake zimeiva.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kukatokea malaika mwingine mwenye uwezo wa kuamuru moto, akatoka kwenye mazabahu, akamwambia kwa sauti kubwa yule aliyekuwa na kisu kikali cha kuvuna: “Nyoosha kisu chako, ukate matunda ya mizabibu yanayokuwa katika dunia kwa maana zabibu zimekomaa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na malaika mwingine akatoka katika ile madhbabu, mwenye mamlaka juu ya moto; kwa sauti kuu akamlilia yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume matawi va mzabibu wa inchi, maana zabibu zake zimewiva sana.