Revelation 14:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sauti iliyokuwa kama ya maji mengi na kama ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sauti ya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kwa kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni yenye kelele kama mafuriko au ngurumo ya radi. Lakini ilisikika kama sauti ya wapiga vinubi wapigao vinubi vyao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sauti iliyokuwa kama sauti ya maji mengi na kama sauti ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sauti ya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sauti iliyokuwa kama ya maji mengi na kama ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sauti ya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi yaendayo kwa kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sauti iliyokuwa kama ya maji mengi na kama ya ngurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sauti ya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikasikia sauti toka mbinguni kama uvumi wa maji mengi na kama uvumi wa ngurumo kuu. Hizo sauti, nilizozisikia, zilikuwa kama za wapiga mazeze, wakiyapiga mazeze yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikinguruma kama uvumi wa maporomoko ya maji mengi na kama ngurumo kubwa ya radi. Sauti ile ilisikilika kama vile sauti ya wapiga vinubi wakati wanapopiga vinubi vyao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama santi ya maji mengi na kama sauti ya radi kuu. Nikasikia sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao: