Revelation 14:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririko wenye kina kufikia hatamu za farasi na urefu upatao kilomita 300.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasi, kwa umbali wa maili mia moja na themanini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Zabibu zikaminywa kwenye shinikizo nje ya mji. Damu ikatiririka kutoka kwenye shinikizo, ikanyanyuka juu kama vichwa vya farasi kwa urefu wa kilomita mia tatu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririko mrefu kiasi cha mita mia tatu na kina chake kiasi cha mita mia mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririko wenye kina kufikia hatamu za farasi na urefu upatao kilomita 300.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka katika hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasi, kwa umbali wa maili 200.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasi, kwa umbali wa maili 200.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririko wenye kina kufikia hatamu za farasi na urefu upatao kilomita 300.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo humo kamulioni zikakamuliwa nje ya mji, ndipo, humo kamulioni mlipotoka damu, ikapajaa, ikafika mpaka penye hatamu za farasi; mtu akipazunguka ni mwendo wa siku mbili mchana kutwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zile zabibu zikakamuliwa mbali na muji, damu ikatiririka toka ndani ya kile kikamulio mpaka ikafika kwenye umbali wa kilometre yapata mia tatu. Nao urefu kwenda chini wa ile damu ulikuwa yapata metre moja na nusu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka khatamu za farasi, mwendo wa mastadio elfu na sita mia.