Revelation 14:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu 144,000 waliokombolewa duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi, na mbele ya wale viumbe wanne wenye uhai, na wale wazee. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao elfu mia moja na arobaini na nne waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu waliimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na viumbe wenye uhai wanne na wazee. Walioujua wimbo mpya ni wale 144,000 tu walionunuliwa kutoka duniani. Hakuna mwingine tena aliyekuwa anaujua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu mia moja arobaini na nne elfu waliokombolewa duniani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu 144,000 waliokombolewa duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Hakuna mtu ye yote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wanne wenye uhai na wale wazee. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale elfu mia moja na arobaini na nne, walionunuliwa katika nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu 144,000 waliokombolewa duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha kifalme penye wale nyama wanne na wale wazee. Hakuwako mtu aliyeweza kujifunza ule wimbo, wasipokuwa wale 144000 waliokombolewa na kuondolewa nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu elfu mia moja makumi ine na ine waliimba wimbo mupya mbele ya kile kiti cha kifalme na mbele ya vile viumbe vine vya ajabu na ya wale wazee. Hakuna mutu aliyeweza kujifunza wimbo ule, isipokuwa wale watu elfu mia moja makumi ine na ine waliokombolewa katika dunia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi.