Revelation 14:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale wanaoishi duniani: kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikaona malaika mwingine akipaa juu angani, akitangaza Habari Njema ya milele kwa watu waishio duniani, watu wa kila taifa, kabila, lugha na rangi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu wote waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote, watu wa lugha zote na rangi zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, akiwa na Injili ya milele, awahubirie hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikamwona malaika mwingine anaruka juu angani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka mbinguni kati na kuushika Utume mwema wa kale na kale wa kuwatangazia nchini wamizimu wote na mashina yote na misemo yote na makabila yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona malaika mwingine akiruka juu sana katika mbingu akiwa na Habari Njema ya milele ya kupasha kwa wakaaji wa dunia, kwa watu wa kila taifa, wa kila kabila, wa kila luga na kila jamaa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikaona malaika niwingine akiruka kati kati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awakhubiri wakaao juu ya inchi na killa taifa na kabila na lugha na jamaa,