Revelation 14:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na dunia, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika akasema kwa sauti kuu, “Mcheni Mungu na msifuni yeye. Wakati wa Mungu kuwahukumu watu wote umefika. Mwabuduni Mungu. Aliumba mbingu, dunia, bahari na chemichemi za maji.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na dunia, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumpa utukufu, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na dunia, bahari na chemchemi za maji.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akasema kwa sauti kuu: Mcheni Mungu na kumtukuza! Kwani saa ya hukumu yake imekuja. Mwangukieni yeye aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akasema kwa sauti kubwa: “Mumuheshimu Mungu na kumutukuza, kwa sababu saa yake ya kuwahukumu watu imetimia. Mumwabudu yule aliyeumba mbingu na dunia, bahari na chemichemi za maji.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, kamtukuzeni, maana saa ya hukumu yake imekuja. Kamsujuduni yeye aliyezifanya mbingu na inchi na bahari na chemchemi za maji.