Revelation 14:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, “Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake — divai kali ya uzinzi wake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa pili akafuata akisema, “Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu, mji ule ulioyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha malaika wa pili akamfuata malaika wa kwanza na kusema, “Ameteketezwa! Mji mkuu Babeli umeteketezwa! Aliwafanya mataifa yote kunywa mvinyo wa uzinzi wake na ghadhabu ya Mungu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, “Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake—divai kali ya uzinzi wake!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, “Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake — divai kali ya uzinzi wake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa pili akafuata akisema, “Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa pili akafuata akisema, “Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu, ule uliyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika wa pili alimfuata huyo wa kwanza akisema, “Ameanguka! Naam, Babuloni mkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifa yote wainywe divai yake – divai kali ya uzinzi wake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakafuata mwingine, ni malaika wa pili, akasema: Umeanguka! Umeanguka mji mkubwa wa Babeli uliowanywesha wamizimu wote mvinyo ya ugoni wake itokezayo makali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa pili akafuata yule wa kwanza akisema: “Umebomoka, umebomoka kabisa, ule muji mukubwa Babeli. Umewakunywesha mataifa yote divai yake kali, ukiwalewesha na maovu ya uasherati wake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika mwingine akamfuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya hasira ya uasharati wake.