Revelation 15:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni: malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo nikaona ajabu nyingine mbinguni, ilikuwa kubwa na ya kushangaza. Walikuwepo malaika saba wenye mapigo saba. Haya ni mapigo ya mwisho kwa sababu baada ya haya, ghadhabu ya Mungu itakuwa imekwisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa makubwa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo makubwa saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni, malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni: malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaona kielekezo kingine mbinguni kilicho kikubwa cha kustaajabu, ni malaika saba walioyashika mapigo saba ya mwisho, kwani katika hayo ndimo, makali ya Mungu yalimotimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona tena katika mbingu kitambulisho kingine kikubwa na cha kushangaza sana. Kulikuwa wamalaika saba wanaoshika mapigo saba. Mapigo haya ndiyo yaliyokuwa ya mwisho, kwa maana ni yale Mungu atakayotumia kwa kutimiza kasirani yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NIKAONA ishara nyingine katika mbingu, kubwa, ya ajabu, malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo hasira ya Mungu imetimia.