Revelation 15:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wa Mwanakondoo: “Bwana Mungu Mwenye Nguvu, matendo yako ni makuu na ya ajabu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wakaimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema: “Bwana Mungu Mwenyezi, matendo yako ni makuu na ya ajabu. Njia zako wewe ni za haki na za kweli, Mfalme wa nyakati zote!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waliuimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwanakondoo: “Mambo unayotenda ni makuu na ya kushangaza, Bwana Mungu Mwenye Nguvu. Njia zako ni sahihi na za kweli, mtawala wa mataifa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo: “Bwana Mungu Mwenye Uwezo, matendo yako ni makuu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wa Mwanakondoo: “Bwana Mungu Mwenye Nguvu, matendo yako ni makuu na ya ajabu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo wakisema: “BWANA Mungu Mwenyezi, matendo yako ni makuu na ya ajabu. Njia zako wewe ni za haki na za kweli Mfalme wa nyakati zote!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wakaimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema: “ bwana Mwenyezi Mungu, matendo yako ni makuu na ya ajabu. Njia zako wewe ni za haki na za kweli, Mfalme wa nyakati zote!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikuwa wakiimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wa Mwanakondoo: “Bwana Mungu Mwenye Nguvu, matendo yako ni makuu na ya ajabu mno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na za kweli!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaimba wimbo wa Mose aliyekuwa mtumwa wake Mungu na wimbo wa Mwana kondoo wakisema: Kazi zako ni kuu na za kustaajabu, Bwana Mungu Mwenyezi! Njia zako ni za wongofu na za kweli, mfalme wa wamizimu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliimba wimbo wa Musa, mutumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana- Kondoo wakisema: “Ewe Bwana wetu, Mungu Mwenye Uwezo, matendo yako ni makubwa na ya ajabu! Ewe Mufalme wa mataifa, kazi zako ni za haki na za kweli!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.