Revelation 15:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa na kanda za dhahabu vifuani mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndani ya lile Hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani iliyong’aa, na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung'aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kisha malaika saba wenye mapigo saba wakatoka nje ya hekalu. Walikuwa wamevaa kitani safi inayong'aa. Wamevaa mikanda mipana ya dhahabu vifuani mwao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa, na kanda za dhahabu vifuani mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa na kanda za dhahabu vifuani mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndani ya lile Hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani ing'aayo na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndani ya lile hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani ing’aayo na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung'aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa na kanda za dhahabu vifuani mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Humo Jumbani mwa Mungu wakatoka wale malaika saba; walioyashika yale mapigo saba; walikuwa wamevaa nguo nyeupe zimetukazo, napo vifuani walikuwa wamefunga mikanda ya dhahabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wale wamalaika saba walioshika mapigo saba wakatoka katika lile hekalu. Walikuwa wamevaa nguo zilizofumwa na nyuzi za pamba zenye kungaa na mikaba ya zahabu katika viuno vyao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakaloka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, kingʼaacho, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.