Revelation 15:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia hekaluni mpaka mwisho wa mabaa saba ya wale malaika saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nalo lile Hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna yeyote aliyeweza kuingia mle Hekaluni hadi yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hekalu lilikuwa limejaa moshi uliotoka katika utukufu na nguvu ya Mungu. Hakuna ambaye angeweza kuingia hekaluni mpaka mapigo saba ya malaika saba yamemalizika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwa saba ya wale malaika saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia hekaluni mpaka mwisho wa mabaa saba ya wale malaika saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nalo lile Hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna ye yote aliyeweza kuingia mle Hekaluni mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nalo lile hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna yeyote aliyeweza kuingia mle hekaluni mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, mpaka yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia hekaluni mpaka mwisho wa mabaa saba ya wale malaika saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Jumba la Mungu likajaa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na kwenye uwezo wake. Hakuwako hata mmoja aliyeweza kuingia Jumbani mwa Mungu, mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yatakapotimilika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hekalu likajaa moshi kutokana na utukufu wa Mungu na uwezo wake. Na hakuna mutu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu mpaka yale mapigo yaliyoletwa na wale wamalaika saba yalipotimizwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hekalu ikajazwa moshi uliotoka kwa utukufu wa Mungu na uweza wake. Na hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu hatta yatakapotimizwa mapigo saba ya wale malaika saba.