Revelation 16:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, malaika wa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwao Eufrate. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ikawekwa kwa ajili ya wafalme kutoka mashariki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Frati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme kutoka Mashariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa sita akaimimina bakuli yake juu ya mto mkuu Frati. Maji yaliyokuwa mtoni yakakauka. Hili likaandaa njia kwa ajili ya watawala kutoka mashariki kuweza kupita.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika wa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwao Eufrate. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ilitengenezwa kwa ajili ya wafalme wa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, malaika wa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwao Eufrate. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ikawekwa kwa ajili ya wafalme kutoka mashariki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Eufrati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme watokao Mashariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Frati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme watokao Mashariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika mawio ya jua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, malaika wa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwao Eufrate. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ikawekwa kwa ajili ya wafalme kutoka mashariki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wa sita alipokimwaga chano chake mle katika mto mkubwa wa Eufurati, ndipo, maji yake yalipokupwa, kusudi njia itengenezwe ya wafalme watakaotoka maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa sita akamwanga kikombe chake katika muto mukubwa Furati. Maji yake yakakauka kusudi njia itengenezwe kwa ajili ya wafalme wanaotoka mashariki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa sita akakimimina kichupa chake juu ya mto ule mkubwa Eufrate, maji yake yakakauka illi njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.