Revelation 16:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama na kinywani mwa yule nabii wa uongo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nikaona roho chafu tatu zilizoonekana kama vyura. Walitoka katika kinywa cha joka, kinywa cha mnyama, na kinywa cha nabii wa uongo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama, na kinywani mwa yule nabii wa uongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama na kinywani mwa yule nabii wa uongo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha lile joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikaona pepo wabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywani mwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama na kinywani mwa yule nabii wa uongo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaona pepo tatu zenye uchafu, zikitoka domoni mwa yule joka namo domoni mwa yule nyama namo domoni mwa yule mfumbuaji wa uwongo, zikawa kama vyura;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu nikaona pepo wachafu watatu wanaofanana na vyura wakitoka ndani ya kinywa cha yule nyoka mukubwa, na ndani ya kinywa cha yule nyama wa ajabu na cha yule nabii wa uongo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikaona roho tatu za uchafu kama vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule nyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo.