Revelation 16:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita ya ile siku kubwa ya Mungu Mwenye Nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho hizi chafu ni roho za mapepo. Zina nguvu za kutenda miujiza. Nazo huenda kwa watawala wa ulimwengu wote na kuwakusanya kwa ajili ya mapigano siku ile Mungu Mkuu Mwenye Nguvu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita kuu Siku ile ya Mungu Mwenye Uwezo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita ya ile siku kubwa ya Mungu Mwenye Nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawa ndio roho za pepo wafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili ya vita ya ile siku kubwa ya Mungu Mwenye Nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani ndizo roho za pepo zinazofanya vielekezo. Zikawatokea wafalme wa ulimwengu wote, ziwakusanye kupiga vita, siku kubwa ya Mungu Mwenyezi itakapotimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawa ndio pepo wanaoonyesha vitambulisho. Nao ndio wanaokwenda kwa wafalme wote wa dunia na kuwakusanya kwa kupigana vita Siku ile kubwa ya Mungu Mwenye Uwezo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi.