Revelation 16:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sikiliza! Mimi naja kama mwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaa nguo zake ili asije akaenda uchi huko na huko na kuaibika hadharani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tazama, naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Sikilizeni! Nitakuja kama mwizi wakati msioutarajia. Heri watakaokuwa macho na waliovaa nguo zao. Hawatakwenda wakiwa uchi na kuona aibu watakapoonwa na watu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Sikiliza! Mimi naja kama mwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaa nguo zake ili asije akaenda uchi huko na huko mbele ya watu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sikiliza! Mimi naja kama mwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaa nguo zake ili asije akaenda uchi huko na huko na kuaibika hadharani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tazama, naja kama mwivi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tazama, naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(Tazama, naja kama mwizi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sikiliza! Mimi naja kama mwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaa nguo zake ili asije akaenda uchi huko na huko na kuaibika hadharani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama, ninakuja kama mwizi. Mwenye shangwe ndiye atakayekesha na kuziangalia nguo zake, asitembee mwenye uchi, watu wakiyaona yake yenye soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sikiliza, ninakuja kwa saa isiyozaniwa kama vile mwizi. Heri yule anayekesha na kutunza nguo zake vizuri kusudi asitembee uchi na kujifezehesha mbele ya watu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake.