Revelation 16:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, hekaluni, ikisema, “Imetendeka!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle Hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa saba akaimimina bakuli yake angani. Sauti kuu ikatoka hekaluni katika kiti cha enzi. Ikasema, “Imekwisha!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, Hekaluni, ikisema, “Mwisho umefika!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, hekaluni, ikisema, “Imetendeka!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle Hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo wa saba akalimimina bakuli lake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, hekaluni, ikisema, “Imetendeka!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wa saba alipokimwaga chano chake angani, ndipo, sauti kuu ilipotoka Jumbani mwa Mungu upande wa kiti cha kifalme ikisema: Imekwisha kufanyika!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa saba akamwanga kikombe chake katika anga. Halafu sauti kubwa ikasikilika kutoka katika hekalu kwenye kiti cha kifalme ikisema: “Sasa ni mwisho!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.