Revelation 16:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kukatokea umeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapata kutokea tangu Mungu alipomuumba mtu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kukawa na miali ya radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawahi kuwa na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, kwani lilikuwa tetemeko kubwa ajabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha kukawa na mwako wa radi, kelele, ngurumo za radi na tetemeko kuu la nchi. Hili lilikuwa tetemeko kuu kuwahi kutokea tangu watu walipokuwepo duniani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kukatokea umeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapata kutokea tangu Mungu alipomuumba mtu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kukatokea umeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapata kutokea tangu Mungu alipomuumba mtu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kukawa na mianga ya umeme wa radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kukawa na mianga ya umeme wa radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapajawa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kukatokea umeme, kelele, ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapata kutokea tangu Mungu alipomuumba mtu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kukapiga umeme na uvumi na ngurumo, kisha kukawa tetemeko kubwa la nchi kupita yote yaliyokuwapo; tangu hapo, mtu alipokaa nchini, halikuwapo tetemeko lililokuwa kubwa kama hilo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kukatokea umeme, makelele, ngurumo ya radi na tetemeko kubwa la inchi lisilotokea bado tangia watu walipoanza kuishi katika dunia. Kweli tetemeko lile lilikuwa kubwa sana!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Pakawa sauti na radi na umeme, na palikuwa tetemeko la inchi, kubwa, ambalo tangu wana Adamu kuwako juu ya inchi halikuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.