Revelation 16:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mji ule mkuu ukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikateketea. Babuloni, mji mkuu, haukusahauliwa na Mungu. Aliunywesha kikombe cha divai ya ghadhabu ya hasira yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akakumbuka Babeli Mkuu na kumpa kikombe kilichojaa mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mji mkuu ukagawanyika vipande vitatu. Miji ya mataifa ikaharibiwa. Na Mungu hakusahau kuuadhibu Babeli Mkuu. Aliupa mji ule kikombe kilichojaa mvinyo wa ghadhabu yake kuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mji ule mkuu ukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikateketea. Babuloni, mji mkuu, haukusahauliwa na Mungu. Aliunywesha kikombe cha divai ya ghadhabu yake kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mji ule mkuu ukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikateketea. Babuloni, mji mkuu, haukusahauliwa na Mungu. Aliunywesha kikombe cha divai ya ghadhabu ya hasira yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akaukumbuka Babeli ule uliokuwa mkuu na kuupa kikombe cha hasira na ghadhabu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akaukumbuka Babeli Mkuu na kumpa kikombe kilichojaa mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mji ule mkuu ukagawanyika katika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mji ule mkuu ukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikateketea. Babuloni, mji mkuu, haukusahauliwa na Mungu. Aliunywesha kikombe cha divai ya ghadhabu ya hasira yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, ule mji mkubwa ulipogawanyika kuwa mafungu matatu, hata miji ya wamizimu ikaanguka. Ndipo, nao mji mkubwa wa Babeli ulipokumbukwa mbele ya Mungu, upewe kinyweo cha mvinyo chungu ya makali yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ule muji mukubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, na miji ya mataifa yote ikabomoka. Mungu hakusahau muji mukubwa Babeli, akaukunywesha kikombe kinachokuwa na divai ya kasirani yake kali.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.