Revelation 16:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama na wale walioiabudu sanamu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa kwanza akaondoka. Akaimimina bakuli yake duniani. Ndipo wale wote waliokuwa na alama ya mnyama na walioiabudu sanamu yake wakapata majipu mabaya yenye maumivu makali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama, na wale walioiabudu sanamu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama na wale walioiabudu sanamu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaenda huyo wa kwanza, akalimimina bakuli lake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juu ya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sana yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama na wale walioiabudu sanamu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakaondoka wa kwanza, akakimwaga chano chake nchini. Ndipo, majipu maovu na mabaya yalipowatokea hao waliokuwa na chapa cha yule nyama, nao waliokiangukia kinyago chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa kwanza akamwanga kikombe chake katika dunia. Halafu majipu mabaya na yenye kuumiza sana yakaota juu ya watu waliokuwa na chapa ya yule nyama na walioabudu sanamu yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake.